SOKA-SIMBASC-MTIBWA SUGAR

Simba yaishinda Mtibwa na kutwaa ngao ya hisani Tanzania

Wachezaji wa Simba wakishangilia katika moja ya michezo ya Ligi Kuu ya Tanzania
Wachezaji wa Simba wakishangilia katika moja ya michezo ya Ligi Kuu ya Tanzania The Citizen

Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2018/19 umefunguliwa rasmi hii leo kwa mchezo wa ngao ya hisani baina ya Simba na Mtibwa Sugar. 

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo umemalizika kwa Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 ambayo yote yalifungwa kipindi cha kwanza cha mchezo.

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na Hassan Dilunga wakati bao la kufutia machozi la Mtibwa lilifungwa na mshambuliaji Kelvin Sabato.

Hili ni taji la kwanza la Simba tangu ilipoanza kunolewa na Kocha Mbelgiji Patrick Aussems.