SOKA-AMAVUBI-AFCON

Kocha mpya Amavubi aahidi kuipaisha Rwanda

Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Vicent mashami
Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Vicent mashami NewTimes

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Vincent Mashami amesema yu tayari kuimarisha hali ya ushindi katika kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' siku chache baada ya kuthibitishwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mashami ametoa kauli hiyo baada ya kuanza kazi ya kuinoa Amavubi akichukua nafasi ya Antoine Hey ambaye aling’atuka mapema mwaka huu baada ya Rwanda kufanya vibaaya katika fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani zilizofanyika nchini Morocco.

Kibarua cha kwanza cha Mashami kitakuwa ni mchezo dhidi ya Ivory Coast wa Kundi H wa kufuzu fainali za Afrika, septemba 9 Mjini Kigali.