MICHEZO-SERENA WILLIUMS

Serena aongoza orodha ya wanamichezo wanawake matajiri duniani

Nyota wa mchezo wa tenisi kwa wanawake duniani, Serena Williums
Nyota wa mchezo wa tenisi kwa wanawake duniani, Serena Williums Aaron Doster-USA TODAY Sports

Orodha ya wanamichezo 10 tajiri duniani kwa upande wa wanawake imewekwa hadharani huku wachezaji nane ya tenisi wakiingia kwenye orodha hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ufatiti uliofanywa na jarida la Forbes unaonyesha Serena Williums anaongoza kwa kuwa na utajiri wa milioni 18 katika kioindi chote alichocheza mchezo wa tenisi.

Caroline Wozniacki anashika nafasi ya pili akiwa na utajiri wa dola milioni 13 wakati wachezaji wengine walioingia kwenye tano bora ni Sloane Stephens, Garbine Muguruza na Maria Sharapova.