SOKA-HISPANIA-REAL MADRID

Umoja wa wachezaji wa Ligi ya Hispania kujadili pendekezo la mechi za ligi hiyo kuchezwa nje ya Ulaya

Nyota wa Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona
Nyota wa Mabingwa wa Hispania, FC Barcelona Reuters/Albert Gea

Wachezaji wa klabu zinazoshiriki ligi kuu ya Hispania wanakutana leo kujadili mpango wa michezo kadhaa ya Ligi hiyo kuchezwa nje ya Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Siku kadhaa zilizopita, maofisa watendaji wa Shirikisho la soka nchini Hispania walitangaza kwamba baadhi ya mechi za Ligi hiyo zitachezwa nchini Marekani na Canada.

Muungano wa wachezaji wa Ligi ya Hispania,(AFE) unasema haukushirikishwa katika mpango huo. Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos na nahodha msaidizi wa Barcelona, sergio Busquets ni miongoni mwa wachezaji wanaohudhuria tukio hilo.

Wachezaji hao wanasema walipaswa kushirikishwa kabla ya kuafikiwa kwa uamuzi huo, na ambao ungelikuwa na manufaa kwa pande zote.

Hata hivyo shirikisho la soka nchini Hispania bado halijatangaza mechi hizo.