SOKA-CECAFA-CAF-FIFA-AFCON

Serengeti Boys yanyakua ushindi wa tatu michuano ya kufuzu Afcon, kanda ya Cecafa

Kikosi cha Serengeti Boys kilichecheza mechi za kuwania kufuzu fainali za Afrika Jijini Dar es salaam
Kikosi cha Serengeti Boys kilichecheza mechi za kuwania kufuzu fainali za Afrika Jijini Dar es salaam Instagram/Serengeti Boys

Timu ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 imetwaa ushindi wa tatu wa michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, kanda ya Cecafa baada ya kuitandika Rwanda kwa penati 4-3.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo umepatikana baada ya timu hizo kufungana mabao 2-2 katika dakika 90 za mchezo.

Tanzania ambayo ilikuwa mwenyeji wa michuano hiyo inayofikia tamati leo, itaungana na mshindi wa mchezo baina ya Ethiopia na Uganda ambazo zinachuana jioni hii katika mchezo wa fainali.

Mchezo huo ulikuwa wa pande zote ambapo timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu.

Mchezo wa fainali unachezwa jioni hii baina ya Ethiopia na Uganda.