VOLIBOLI-MICHEZO

Mashindano ya mchezo wa voliboli kwa wanawake chini ya miaka 20 Kenya

Kenya, Mabingwa wa Volley-ball Afrika mnano mwaka 2015.
Kenya, Mabingwa wa Volley-ball Afrika mnano mwaka 2015. Courtesy of CAVB

Mataifa ya Afrika, yanapambana kwa siku ya pili katika mashindano ya mchezo wa voliboli kwa wanawake chini ya miaka 20, inayoendelea jijini Nairobi nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Nigeria watachuana na Cameroon, Congo dhidi ya Misri na Rwanda itamenyaa na Mauritius.

Wenyeji Kenya, walianza vema baada ya kuwashinda majirani wao kwa seti za 3-0( 25-15, 25-21, 25-11).

Matokeo mengine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliishinda Mauritius kwa seti 3-0 (25-23, 25-18, 25-23).

Siku ya Jumanne, Cameroon itachuana na Tanzania, Misri na Rwanda lakini pia Uganda watamenyana na Congo.

Ratiba ya Jumatano:- Nigeria dhidi ya Kenya, Rwanda dhidi ya Uganda lakini Mauritius dhidi ya Misri.

Mashindano haya, yatamalizika tarehe 3 mwezi Septemba.