UGANAD-ETHIOPIA-SOKA

Uganda yaiadhibu Ethiopia 3-1

Uganda yaendelea kupiga hatua katika masuala ya soka.
Uganda yaendelea kupiga hatua katika masuala ya soka. RFI/Pierre René-Worms

Uganda itaungana na wenyeji Tanzania, kuwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika baina ya vijana wasiozidi miaka 17, itakayopigwa jijini Dar es salaam mwaka 2019.

Matangazo ya kibiashara

Vijana wa Uganda, walipata nafasi hiyo baada ya kuishinda Ethiopia mabao 3-1 katika fainali ya mataifa ya CECAFA, iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salaam.

Abdulwahid Iddi, aliifungia Uganda mabao 2 huku Samson Kasozia akianza kwa kutikisa nyavu za Ethiopia katika dakika ya 14.

Bao pekee la Ethiopia, lilitiwa kimyani na Mintestot Wakjira kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 92 ya mchuano huo.

Wenyeji Tanzania, Cameroon, Uganda na Angola, tayari ni nchi ambazo zimefuzu.

Mwakilishi wa Afrika Kaskazini, na wawakilishi watatu kutoka Afrika Magharibi, wanasubiriwa kufuzu katika michuano hii.

Mataifa manane, yanatarajiwa kushiriki katika michuano hii itakayochezwa kati ya tarehe 12 na 26 mwezi Mei.