KOMBE LA SHRIKISHO-SOKA

Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika yaendelea

Klabu ya kenya ya Gor Mahia itamenyana na USM Algers Jumatatno Agosti 29, 2018.
Klabu ya kenya ya Gor Mahia itamenyana na USM Algers Jumatatno Agosti 29, 2018. gormahiafc.co.ke

Michuano ya taji la shirikisho ngazi ya klabu barani Afrika inafikia taamati wiki hii kwa michezo mbalimbali kuchezwa. Katika kundi D Rayon Sports ya Rwanda, Jumatano itaipokea Yanga ya Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo mwingine wa kundi hilo utakaochezwa Jumatano ni baina ya USM Algers ya Algeria ambayo itachuana na Gor Mahia ya Kenya.

Gor Mahia imeondoka nchini Kenya Jumatatu asubuhi kuelekea Algeria bila mchezaji wake muhimu Jack Tuyisenge anayesumbuliwa na majeraha.

Mechi nyingine AS Vita Club ya DRC itakuwa mwenyeji wa Adouana Stars ya Ghana.

RS Berkane na Al Masry tayari zimefuzu hatua ya robo fainali na timu nyingine zitakazofuzu robo fainali zitajulikana siku ya Jumatano.