UINGEREZA-SOKA

Tottenham yaiadhibu Man Utd 3-0, Jose Mourinho aomba kuhamishwa

Harry Kane wa Tottenham akisherehekea bao lake la kwanza dhidi ya Machester United.
Harry Kane wa Tottenham akisherehekea bao lake la kwanza dhidi ya Machester United. Action Images via Reuters / Andrew Couldridge

Mashetani wekundu Manchester United walikubali kusalimu amri baada ya kuchapwa na Tottenham Hotspurs 3-0 katika uwanja wa Old Trafford.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo uliaanza saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki na ulikuwa mchezo wa tatu kwa timu zote mbili ambapo United ilishinda mechi moja na kupoteza moja wakati Spurs iimekua ikitafuta ushindi wa tatu mfululizo baada ya kushinda mechi mbili za awali.

Bao la kwanza la Tottenham lilifungwa na Harry Kane dakika ya 50 kwa kichwa na Lucas Moura akaweka kimyani bao la pili muda mfupi baadaye kutokana na pasi ya Christian Eriksen.

Lucas Moura alimalizia kwa kufunga bao la tatu dakika sita kabla ya mechi kumalizika na kukamilisha ushindi wa Tottenham Spurs.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema alikuwa na matumani kwamba vijana wke wangejikwamua kutoka kwa uchezaji mbaya uliochangia kuchapwa kwao ugenini na Brighton.

Kipigo hicho cha Jumatatu usiku ndio kikubwa zaidi kwa Machester United wakiwa uwanja wa nyumbani toka na tangu Morinho aanze maisha yake ya ukocha, na pia kwa mara ya kwanza amepoteza michezo miwili kati ya mitatu ya mwanzo ya ligi.

Akihojiwa na waandishi wa habari Jose Morinho amesema "Nimeshinda mataji mengi ya ligi ya EPL kuliko makocha wote 19 (wa timu nyengine zinazoshiriki EPL) ukiwaweka pamoja," huku akiongeza "Nimeshinda mataji matatu na wao mawili."

Mourinho, raia wa Ureno amenyenyua taji la EPL mara tatu kwa vipindi viwili tofauti akiwa na Chelsea, wakati Pep Guardiola na Manuel Pellegrini wakishinda mara moja kila mmoja wakiwa na Manchester City.

Siku ya Jumapili Chelsea iliishinda Newcaste mabao 2-1 na kuchukua hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo ikitanguliwa na Liverpool, zote zina alama tisa.