CAF-KLABU BINGWA-SHIRIKISHO

CAF: Klabu zilizofuzu hatua ya robo fainali zafahamika

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydada Cassablanca ya Morocco katika mechi iliyopita ya klabu bingwa barani Afrika
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydada Cassablanca ya Morocco katika mechi iliyopita ya klabu bingwa barani Afrika www.cafonline.com

Klabu nane zilizofuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kumalizika kwa michuano ya hatua ya makundi siku ya Jumanne usiku.

Miongoni mwa klabu zilizofuzu ni pamoja na Al-Ahly ya Misri na Esperance de Tunis ya Tunisia kutoka kundi A.

Kundi B, mabingwa wa zamani TP Mazembe wajikatia tiketi baada ya kuongoza kwa alama 12 huku ES Setif ya Algeria ikifuzu pia baada ya kuishinda MC Alger pia ya Algeria baada ya kushinda mechi ya mwisho kwa alama 2-1.

Horoya ya Guinea, licha ya kutofungana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, imejiunga na mabingwa watetezi Wydad Casablanca ya Morocco kutoka kundi C.

Etoile du Sahel ya Tunisia na Primero de Agosto ya Angola, yamefuzu kutoka kundi D, huku Zesco ya Zambia ikishindwa kufuzu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Etoile du Sahel katika uwanja wa Levy Mwanawasa.

Droo ya hatua ya robo fainali itachezwa tarehe tatu mwezi Septemba.