KENYA-GHANA-SOKA

Harambee Stars kumkosa Wanyama katika mechi yake dhidi ya Ghana

Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars.
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars. youtube

Kiungo wa Kati wa klabu ya Tottehham Hotspurs Victor Wanyama , hatakuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, wakati Harambee Stars itakapomenyana na Ghana siku ya Jumamosi, jijini Nairobi, katika mechi muhimu ya hatua ya makundi kufuzu katika fainali ya Afrika mwakani nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Tayari kocha Sebastien Migne amekitaja kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 24, na Wanyama ambaye amekuwa nahodha wa Harambee Stars kwa muda mrefu hajajumuishwa.

Wanyama amekuwa akisumbuliwa na jeraha na hata klabu yake haikuwa tayari kumruhusu kuja kuichezea nchi yake.

Badala yake, kocha Migne anatarajiwa kumteua mchezaji mmoja kati ya Francis Kahata, Abdallah Hassan, Anthony Akumu, Eric Johanna, Ismail Gonzalez na Johanna Omollo kuchukua nafasi ya Wanyama.

Kikosi cha timu ya taifa ya Kenya hiki hapa :

Makipa

Patrick Matasi, Farouk Shikalo, Ian Otieno.

Mabeki

Philemon Otieno, Jockins Atudo, Dennis Odhiambo, Joash Onyango, Benard Ochieng, Abud Omar, David Ochieng, Eric Ouma, Joseph Okumu, Musa Mohammed, David Owino.

Viungo wa Kati

Francis Kahata, Abdallah Hassan, Anthony Akumu, Eric Johanna, Ismail Gonzalez, Johanna Omollo.

Washambuliaji

Piston Mutamba, Jesse Were, Michael Olunga, Ovella Ochieng.

............