DRC-SOKA

Leopards wajiandalia mechi yao muhimu siku ya Jumapili

Timu ya taifa ya DRC «Léopards» wakati wa michuano ya AFCON 2017.
Timu ya taifa ya DRC «Léopards» wakati wa michuano ya AFCON 2017. RFI/Pierre René-Worms

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ipo jijini Monrovia nchini Liberia, kwa maandalizi ya mchuano muhimu kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza leo, kikosi hicho cha wachezaji 22 kimeanza kufanya mazoezi pamoja.

Hata hivyo, kikosi cha kocha Florent Ibenge kitawakosa wachezaji wanne ambao wana majeraha ambao ni Yannick Yala Bolasia, Neeskens Kebano, Arthur Masuaku na Jordan Ikoko.

Kipa Ley Matampi Mvumi, hatakuwepo katika mchuano huo muhimu siku ya Jumapili kwa sababu klabu yake ya TP Mazembe haikumpa nafasi ya kuondoka kwa wakati na sasa nafasi yake imechukuliwa na Joel Kiassumbua.

Kikosi cha timu ya taifa ya DRC, Leopards:

Kiassumbua Joël (Servette / Uswizi)

Mossi Ngawi Anthony (Chiasso FC / Uswizi)

Mabruki Nathan (DCMP / DR Congo)

Issama Mpeko Djos (TP Mazembe / DR Congo)

DjumaShabani Wadol (AS V.Club / RD Congo)

Glody Ngonda Muzinga (AS V.Club / DR Congo)

Moke Abro Wilfred (Koniaspor / Uturuki)

Luyindama Nekadio Christian (Standard Liege / Ubelgiji)

Yannick Bangala Litomb (AS V.Club / DR Congo)

Munganga Omba Nelson (AS V.Club / RD Congo)

Maghoma Jacques (Birmingham City / Uingereza)

Mpoku Ebunge Paul-José (Standard Liege / Ubelgiji)

Ngoma Luamba Fabrice (AS V.Club / RD Congo)

Mubele Ndombe Firmin (Toulouse / Ufaransa)

Kabananga Kalonji Junior (Astana FC / Kazakhstan)

Meschak Elia Lina (TP Mazembe / DR Congo)

Bolingi Mpangi Jonathan (Antwerp /Ubelgiji)

Afobe Tunani Benik (Stoke City / Uingereza)

Assombalanga Britt (Middlesbrough FC / Uingereza)

Akolo Chadrack (Stuttgart / Ujerumani)

Ungenda Muselenge Bodrick (Primeiro d'Agosto / Angola)

Lema mabidi Chikito (Raja Casablanca Club / Morocco)