UGANDA-COTE D'IVOIRE-SOKA

Sand Cranes yajiandaa kumenyana na Cote d'Ivoire

Uganda yashiriki michezo mbalimbali Afrika.
Uganda yashiriki michezo mbalimbali Afrika. Reuters

Timu ya taifa ya soka ya Uganda, Sand Cranes, inayocheza soka ufukweni, imeanza maandalizi ya kumenyana na Cote d'Ivoire kutafuta nafasi ya kufuzu fainali ya Afrika, itakayofanyika nchini Misri mwezi Desemba.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji 16 wameanza mazoezi ya pamoja mjini Entebbe, pembezoni mwa Ziwa Victoria. Mechi hii ya kufuzu itachezwa nyumbani na ugenini.

Tanzania nayo inajiandaa kumenyana na Afrika Kusini, mechi itakayochezwa mwishoni mwa juma hili jijini Dar es salaam.

Mataifa nane, yatashiriki katika fainali hizo za bara Afrika na hadi sasa, wenyeji Misri, Libya, Morocco, Nigeria na Senegal tayari yameshafuzu.