AFCON-TAIFA STARS-UGANDA CRANES

Taifa Stars yaibana Uganda, mchezo wa kufuzu Afcon

Beki wa Taifa Stars, David Mwantika akichuana na mshambuliaji wa uganda, Farouk Miya katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika Septemba 8, 2018
Beki wa Taifa Stars, David Mwantika akichuana na mshambuliaji wa uganda, Farouk Miya katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika Septemba 8, 2018 Twitter/FUFA

Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imetoshana nguvu na uganda katika mchezo wa Kundi L wa kuwania kufuzu fainali za Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Mandela uliopo Jijini Kampala, muda mwingi wa kipindi cha kwanza ulitawaliwa na Uganda.

Washambuliaji Emmanuel Okwi na Farouk Miya hata hivyo walishindwa kuweka mpira wavuni kutokana na umakini wa safu ya ulinzi ya Tanzania iliyokuwa ikiongozwa na Agrey Morris.

Kipindi cha pili Tanzania iliongeza uhai na kufanikiwa kufanya mashambulizi katika lango la Cranes lakini umakini wa kipa ,Dennis Onyango uliinyima Tanzania nafasi ya kupata bao la ushindi.

Mvua iliyonyesha jijini Kampala iliathiri hali ya uwanja na kusababisha timu zote mbili kushindwa kumiliki mpira kikamilifu.

Kwa matokeo hayo Uganda inaendelea kuongoza Kundi L ikiwa na alama 4 ikifuatiwa na Tanzania yenye alama mbili.

Mchezo mwingine wa Kundi L unachezwa hivi leo baina ya Cape Verde na Lesotho.

Katika mchezo wa kundi F, Kenya iliinyuka Ghana bao 1-0 na kufikisha alama tatu katika kundi hilo ambalo pia lina timu za Ethiopia na Sierra Leone

Cameroon ilibanwa mbavu na Comoro kwa sare ya bao 1-1

Nigeria iliishinda Ushelisheli kwa mabao 3-0

Misri iliizaba Niger mabao 6-0

Burundi na Gabon zilifungana bao 1-1

Afrika Kusini ilitoka sare ya bila kufungana na Libya

Mechi za Leo ni kama ifuatavyo

Rwanda inachuana na Ivory Coast

Liberia inaipokea DR Congo

Sudani Kusini inachuana na Mali

Ethiopia inacheza na Sierra Leone