AFCON 2019-AFRIKA-CAMEROON-CAF-SOKA

Kenya yaishinda Ghana,Uganda na Tanzania zatoshana nguvu

Michael Olunga akishangilia goli, alilosaidia nchi yake kupata wakati Kenya ikimenyana na Ghana Septemba 08 2018 katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi
Michael Olunga akishangilia goli, alilosaidia nchi yake kupata wakati Kenya ikimenyana na Ghana Septemba 08 2018 katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi http://www.cafonline.com/

Michuano ya soka, kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon, iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, imeonesha kuwa hakuna timu ndogo katika safari ya kufuzu katika fainali hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kundi F, ambalo lina Ghana, Kenya, Ethiopia na Sierra Leon, timu zote zina alama tatu baada ya kucheza  mechi mbili.

Hii inamaanisha kuwa timu zote zimepata ushindi mechi moja na kupoteza mchuano mwingine. Hakuna sare iliyoshuhudiwa katika kundi hili.

Matokeo ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Kenya iliishinda Ghana bao 1-0 jijini Nairobi huku Ethiopia ikiifunga Sierra Leon 1-0.

Kundi L, linaongozwa na Uganda ambayo haikufungana na Tanzania katika mechi muhimu iliyochezwa katika uwanja Naambole jijini Kampla.

Uganda inaongoza kundi hili kwa alama 4, huku Lesotho ikiwa na alama 2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Cape Verde. Tanzania pia ina alama mbili katika kundi hili.

Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zina alama 4. Mechi za kundi hili zilimalizika kwa sare. Liberia waliilazimisha sare ya bao 1-1, matokeo yaliyoshuhudiwa pia katika mecho kati a Zimbabwe na Congo Brazaville.

Matokeo mengine:-

Equatorial Guinea 1 vs Sudan 0

Sudan Kusini vs 0 Mali 3

Angola 1 vs Botswana 0

eSwatini 0 vs Tunisia 2

Seychelles 0 vs  Nigeria 3

Comoros 1 vs Cameroon 1

Msumbiji 2 vs Guinea-Bissau 2
 

Mechi zingine  zitachezwa mwezi Oktoba.