RIADHA-MICHEZO

Mashindano ya Riadha ya masafa marefu kupigwa Jumapili

Mwanariadha Mkenya Wilson Kipsang. .
Mwanariadha Mkenya Wilson Kipsang. . REUTERS/Tobias Schwarz

Siku ya Jumapili kutakuwa na Makala ya 45 ya mashindano ya riadha ya masafa mrefu maarufu kama Berlin Marathon. Ni mashindano itakayowashirikisha wanariadha wa kiume na wakike kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Matangazo ya kibiashara

Ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya bingwa mtetezi kwa upande wa wanaume Mkenya Eliud Kipchoge, ambaye anatarajiwa kupata ushindani kutoka kwa Mkenya mwenzake Wilson Kipsang na Zersenay Tadese wa Eritrea na Abera Kuma kutoka Ethiopia.

Lakini swali kubwa ni je, wanaridha hao watavunja rekodi iliyowkew ana Mkenya Dennis Kimeto ya saa mbili, dakika mbili na sekunde 57 mwaka 2014 ?

Kwa upande wa wanawake, ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya bingwa mtetezi, Gladys Cherono kutoka Kenya na mwezake Edna Kiplagat lakini pia Tirunesh Dibaba kutoka Ethiopia.