CAF-SOKA

Taji ya klabu bingwa: Michuano ya hatua ya robo fainali kupigwa

Horoya ya Guinea itakuwa nyumbani kupepetana na Al Ahly ya Misri (kwenye picha).
Horoya ya Guinea itakuwa nyumbani kupepetana na Al Ahly ya Misri (kwenye picha). AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Michuano ya hatua ya robo fainali, kuwania taji ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika, inachezwa mwishoni mwa juma hili. Ijumaa usiku, Horoya ya Guinea itakuwa nyumbani kucheza na Al Ahly ya Misri huku ES Setif ikimenyana na Wydad Casablanca ya Morocco.

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi kuanzia saa saa moja kamili saa za Afrika Mashariki, Primerio de Agosto ya Angola, itamenyana na TP Mazembe ya DRC.

Mechi nyingine itachezwa saa nne usiku kati ya klabu kutoka nchi moja ES Tunis na Etoile du Sahel.

Jumapili, itakuwa ni zamu Shirikisho barani Afrika, CARA Brazaville ya Congo, itachuana na Raja Casablanca, Rayon Sport itakuwa jijini Kigal kucheza na Enyimba ya Nigeria, huku AS Vita Club ikicheza na RSB Berkane ya Morocco. Nayo Al Masry ya Misri itamenyana na USM Alger.

Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini.