RIADHA-ELIUD KIPCHOGE-KENYA

Eliud Kipchoge avunja rekodi ya Dennis Kimetto, Mbio za Marathoni za Berlin

Mwanariadha wa mbio ndefu wa kenya, Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Berlin Marathon
Mwanariadha wa mbio ndefu wa kenya, Eliud Kipchoge akishangilia baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Berlin Marathon Evening Standard

Mwanariadha Mkenya, Eliud Kipchoge amevunja rekodi iliyowekwa miaka minne iliyopita na mkenya mwenzake Denis Kameto katika mashindano ya Marathon ya Berlin. 

Matangazo ya kibiashara

Kipchoge anakimbia masafa ya mbio ndefu kwa kasi duniani.

Mkenya mwenzake Dennis Kameto aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kutumia muda wa saa 2 dakika 2 na sekunde 57.

Nyota huyo wa mbio ndefu amevunja rekodi ya mbio hizo kwa kutimka kilomita 42 kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 40.

Hii ilikua ni mara ya tatu kwa Kipchoge kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za Berlin marathon.Amos Kipruto, Mkenya mwingine alinyakua ushindi wa pili kwa kutumia muda wa saa 2, dakika 6 na sekunde 24, Wilson Kipsang akaibuka wa tatu kwa kutimka kwa saa mbili, dakika 6 na sekunde 48.