TANZANIA-SIMBASC-TFF

Simba yabanwa mbavu, Ligi ya Tanzania

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ni mmoja ya wachezaji watatu wa klabu hiyo walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji borta wa Ligi Kuu
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi ni mmoja ya wachezaji watatu wa klabu hiyo walioteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji borta wa Ligi Kuu GOAL.COM

Mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC jana walibanwa mbavu na kulazimishwa sare ya bila kufungana na Ndanda.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo wa tatu kwa Simba tangu kuanza kwa Ligi ya Tanzania Bara, ulichezwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania. Katika mchezo huo, kwa mara ya kwanza Kocha Patrick Aussems aliwatumia washambuliaji watatu, Meddie Kagere, Emanuel Okwi na John Bocco.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama saba baada ya kucheza mechi tatu.

Matokeo ya mechi nyingine Singida United iliishinda KMC bao 1-0 nayo Tanzania Prisons ilivutwa shati kwa kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Ruvu Shooting.

Mechi kadhaa zinachezwa leo ikiwemo mchezo baina ya Yanga na Singida United ambao unachezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.