AFRIKA-CAF-SOKA

Marefarii zaidi ya 40 kutoka nchi mbalimbali wapewa mafunzo zaidi

Kiongozi wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Ahmad
Kiongozi wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Ahmad KHALED DESOUKI / AFP

Marefarii wa mchezo wa soka zaidi ya 40 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wamemaliza  mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Matangazo ya kibiashara

Mafunzo hayo yaliwaleta pamoja marefarii wachanga waliopimwa afya na kufanya mazoezi ya mwili katika uwanja wa soka wa Namboole.

Moses Magogo rais wa Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA na mwanachama wa Kamati ya CAF na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya marefarii katika Shirikisho hilo la soka barani Afrika An Yan Lim Kee Chong, ni miongoni mwa maafisa wengine, waliosimamia zoezi hilo.

CAF inasema imeamua kutoa mafunzo haya kwa marefarii hao, ili kuendelea kuwapa mafunzo zaidi na kuwakumbusha sheria 17 za mchezo wa soka.