TFF-TANZANIA-AFRICAN LYON

Lionel Soccoia: Kukosekana kwa udhamini kunaathiri Ligi ya Tanzania

Mwandishi wa RFI Kiswahili Ali Bilal (Katikati) akiongoza mahojiano baina ya kocha wa African Lyon Soccoia Lionel na mchezaji Victor Da Costa Tarehe 21 Septemba 2018
Mwandishi wa RFI Kiswahili Ali Bilal (Katikati) akiongoza mahojiano baina ya kocha wa African Lyon Soccoia Lionel na mchezaji Victor Da Costa Tarehe 21 Septemba 2018 RFI Kiswahili/Victor Abuso

Kocha Mkuu wa Timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mfaransa, Soccoia Lionel amesema kukosekana kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu kunaathiri soka la Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya RFI yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Inatuathiri, inatuathiri,japokuwa kwa sasa hatujaona athari zozote lakini mambo yatakuwa magumu mble ya safari.” ameeleza.

Katika hatua nyingine Lionel amesifu uwezo wa wachezaji wa soka kutoka Afrika Mashariki na kati na kudai wanaweza kufika mbali katika michuano mbalimbali ikiwa watazingatia nidhamu na maadili ya soka.

Naye mchezaji Victor Da Costa ambaye anaichezea klabu ya African Lyon amekiri mazingira ya soka la Tanzania ni mazuri na yamemsaidia kujifunza tamaduni na maisha ya waafrika.

“Watanzani ni watu wenye urafiki na watu, ninajifunza mengi,”

Sikiliza mahojiano ya Kocha Saccoia Lionel na RFI Kiswahili