SOKA-FIFA-MODRIC-REAL MADRID-CROATIA

Luka Modric ashinda tuzo ya mchezaji bora duniani

Luka Modric, mchezaji bora wa mwaka 2018
Luka Modric, mchezaji bora wa mwaka 2018 www.fifa.com

Luka Modric, kiungo wa kati anayechezea klabu ya Real Madrid nchini Uhispania na timu ya taifa ya Croatia, ndio mchezaji bora wa mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Modric alishinda tuzo hiyo baada ya kumshinda Cristiano Ronaldo anayechezea klabu ya Juventus na Mohammed Salah kutoka Misri anayechezea klabu ya Liverpool nchini Uingereza aliyeshinda, tuzo ya bao bora la mwaka 2018.

Mchezaji huyo wa Croatia aliisaidia timu yake kufika katika hatua ya fainali ya kombe la dunia licha ya kushindwa na Ufaransa mwezi Julai, lakini pia aliisaidia klabu yake kushinda taji la klabu bingwa barani Ulaya.

Tuzo ya mwaka 2018 ilitolewa katika hafla iliyofanyika jijini London nchini Uingereza Jumatatu usiku.

Kuanzia mwaka 2017 tuzo la FIFA limekuwa likitolewa kwa ushirikiano na lile la Ufaransa la Ballon d'Or na siku hizi hufahamika kama FIFA Ballon d'Or, ushirikiano ambao utaendelea kwa miaka sita.

Orodha kamili ya washindi:

Bao bora la mwaka

Mohamed Salah (Misri & Liverpool)

Kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume

Didier Deschamps (Ufaransa)

Kipa bora

Thibaut Courtois (Ubelgiji & Real Madrid)

Kocha bora kwa upande wa wanawake

Reynald Pedros (Lyon)

Shabiki bora wa mwaka

Mashabiki kutoka Peru, wakati wa kombe la dunia nchini Urusi.

Mchezaji mwenye nidhamu

Lennart Thy (Ujerumani)

Kikosi bora cha wachezaji 11 duniani

David De Gea, Dani Alves, Raphael Varane, Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric, N'Golo Kante, Eden Hazard, Lionel Messi, Kylian Mbappe, Cristiano Ronaldo

Mchezaji bora kwa upande wa wanawake

Marta (Orlando Pride & Brazil)

Mchezaji bora kwa upande wa wanaume

Luka Modric (Croatia & Real Madrid)