TAIFA STARS-CAPE VERDE-AFCON

Amunike aita nyota 30 wa Taifa Stars kuivaa Cape Verde, akiwarejesha kundini nyota wa Simba

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike pulse.ng

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike ametaja majina ya wachezaji 30 wa timu hiyo wakataochuana na Cape Verde mwezi ujao katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Katika kikosi hicho Amunike amewarejesha kundi baadhi ya wachezaji wa Simba ambao mwezi uliopita waliachwa kwenye kikosi cha Stars baada ya kuchelewa kuripoti kambini.

Wachezaji waliorejeshwa kundini ni Jonas Mkude, John Bocco na Shomari Kapombe huku Shiza Kichuya na Hassan Dilunga wakiachwa.

Otoba 12 Tanzania itakuwa mgeni wa Cape Verde kabla ya timu hizo kurudiana siku nne baadaye jijini Dar es Salaam.

Tanzania inashika nafasi ya pili katika Kundi L ikiwa na alama mbili ikitanguliwa na Uganda yenye alama nne.

Kikosi kilichoitwa ni

Makipa

Aishi Manula

Beno Kakolanya

Mohammed Abdulahim

Mabeki

Hassan kessy

Shomari Kapombe

Salum Kimenya

Gadiel Michael

Paul Ngalema

Ally Sonso

Aggrey Morris

David Mwantika

Abdallah Kheri

Kelvin Yondan

Andrew Vicent

Abdi Banda

Viungo

Himid Mao

Simon Msuva

Mudathir Yahya

Frank Domayo

Jonas Mkude

Feisal Salum

Salum Kihimbwa

Farid Mussa

Washambuliaji

Mbwana Samatta

Thomas Ulimwengu

John Bocco

Yahya Zaid

Kelvin Sabato

Rashid Mandawa

Shaaban Chilunda