MANCHESTER UNITED-JOSE MOURINHO-RIO FERDINAND

Ferdinand:Manchester United inapaswa kuchukua uamuzi mgumu

Kocha wa Manchester united, Jose Mourinho
Kocha wa Manchester united, Jose Mourinho Evening Standard

Mchezaji wa safu ya ulizni wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Rio Ferdinand amesema klabu ya Manchester united ina kila sababu ya kufanya uamuzi mgumu kufuatia mwanzo mbaya wa ligi kuu ya England katika kipindi cha miaka 29.

Matangazo ya kibiashara

United imepoteza mechi tatu za Ligi kuu kati ya saba ilizocheza na pia imeondolewa katika michuano ya Carabao na jana ilichapwa mabao 3-1 na West Ham United katika mchezo wa Ligi kuu ya England.

Ferdinand amesema ni lazima klabu hiyo itafikiria mara mbili mustakbali wake baada ya mfululizo wa matoko mabovu.

Mara ya mwisho United kuanza vibaya msimu wa Ligi kuu ya England ilikuwa msimu wa 1989/1990.

United imekusanya alama 10 katika mechi saba za Ligi Kuu ilizocheza na tayari mashabiki wa klabu hiyo wameanza kupaza sauti ya kumtaka Kocha Jose Mourinho ajiuzulu.