SOKA-MBWANA SAMATTA-TANZANIA

Nyota ya Samatta yaendelea kung'ara barani ulaya

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta GOAL.COM

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta jana aliifungia klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji mabao matatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Zulte-Weregen. 

Matangazo ya kibiashara

Genk iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Samatta alifunga mabao hayo katika dakika za 31, 68 na 86 na bao lingine lilifungwa na Pozuelo dakika ya 29 ya mchezo.

Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Samatta kufunga mabao matatu tangu alipojiunga na klabu hiyo Januari 2016 akitokea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Genk inashika nafasi ya pili kwa kuwa na alama 23 ikitanguliwa na Clube Brugge yenye alama 25.

Awali, Samatta aliifungia klabu yake zaidi ya mabao matano katika michezo ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Europa.

Ligi Kuu ya Ubelgiji inashirikisha timu 16 na imekuwa ikitoa wachezaji ambao kwa sasa wanatamba na klabu kubwa za Ulaya akiwemo Romelu Lukaku, Eden Hazzard na Marouane Fellaine.