SENEGAL-OLIMPIKI-2022

Senegal kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki kwa vijana mwaka 2022

Senegal itakuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki kwa vijana, itakayofanyika jijini Dakar mwaka 2022.

Senegal kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki mwaka 2022
Senegal kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki mwaka 2022 NBC Sports/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa na viongozi wa Kamati ya michezo hii IOC, waliokutana jijini Buenos Aires, nchini Argentina.

Senegal ilipata nafasi hiyo baada kuyashinda mataifa mengine ya Afrika kama Bostwana, Nigeria na Tunisia.

Rais wa IOC Thomas Bach amesema, bara la Afrika limeungana na Senegal kufanikisha mashindano hayo, yatakayofanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Dakar litakuwa jiji la tano kuandaa michezo hii tangu kuzinduliwa kwake jijini Singapore mwaka 2010, Nanjing nchini China mwaka 2014, Buenos Aires mwaka 2018.