SOKA-WENGER-MICHEZO

Wenger: Niko tayari kurejea katika kazi yangu ya ukocha mwezi Januari

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger.
Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger. Reuters/Matthew Childs

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal huko nchini Uingereza, Arsene Wenger, anasema anatarajia kurejea kazi kuanzia tarehe moja mwezi Januari.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 68 anasema amepokea maombi mengi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Wenger amekuwa akipumzika, baada ya kustaafu kuifunza Arsenal, klabu aliyoitumikia kwa miaka 22.

Kocha huyo amesema amevutiwa kurejea katika kazi yake baada ya kupata ofa za kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Hata hivyo, amesema hajafahamu atakwenda wapi, lakini amedokeza anaweza hata kwenda kufunza timu ya taifa.

“Ninaamini kuwa nitaanza tena kufundisha Januari mosi. Sijui hasa ni wapi nitafundisha, kwa sasa nimepumzika na nitakuwa tayari kufundisha tena”, amesema Wenger.