EUROPA LEAGUE-UEFA-ULAYA

Mechi za Ligi ya Europa kuchezwa leo barani Ulaya

Nyota wa Arsenal Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang wanatazamiwa kuongoza kikosi cha Arsenal kitakachochuana na Sporting Lisbon ya Ureno
Nyota wa Arsenal Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang wanatazamiwa kuongoza kikosi cha Arsenal kitakachochuana na Sporting Lisbon ya Ureno REUTERS/Eddie Keogh

Michuano ya Europa League kwa ngazi ya klabu inaendelea leo kwa mechi mbalimbali kuchezwa katika Miji tofauti barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo ni ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya, yakitanguliwa na michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

RB Leipzg itakuwa mgeni wa Celtic ya Scotland, Arsenal imesafiri hadi nchini Ureno ambako itachuana na Sporting Lisbon wakati Chelsea ya Uingereza itaipokea BATE Borisov ya Bulgaria.

Mechi nyingine ni kama ifuatavyo.

Rangers itachuana na Spartak Moscow

RB Salzburg itachuana na Rosenburg ya Norway

Zenit St Petersburg itachuana na Bordeaux ya Ufaransa

Anderlect ya Ubelgiji itapambana na Fenerbance ya Uturuki

FC Copenhagen itapambana na Slavia Prague