CAF-SHIRIKISHO-RAJA CASABLANCA-AS VITA

AS Vita Club na Raja Casablanca kumenyana katika fainali ya kuwania taji la Shirikisho

Klabu ya AS Vita Club nchini DRC
Klabu ya AS Vita Club nchini DRC www.cafonline.com

AS Vita Club ya DRC itamenyana na Raja Casablanca ya Morocco katika fainali ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya fainali itachezwa nyumbani na ugenini, tarehe 25 mwezi Novemba na tarehe mbili mwezi Desemba.

Vita Club ilifanikiwa kufika katika hatua hiyo baada ya kuishinda Al Masry ya Misri mabao 4-0 katika mechi ya mzunguko wa pili, hatua ya nusu fainali.

Mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Port Said, timu hizo mbili hazikufungana.

Raja Casablanca nayo ilifuzu baada ya kuishinda Enyimba ya Nigria kwa mabao 3-1.

Enyimba ilipoteza mechi zote, nyumbani ilifungwa bao 1-0 huku ugenini ikifungwa mabao 2-1.