AFCON-RWANDA-DRC

Timu ya Vijana ya Rwanda chini ya miaka 23 yajiwinda na Mechi ya mchujo Afcon

Kocha wa Timu ya Taifa ya vijana ya Rwanda chini ya miaka 23, Jimmy mulisa
Kocha wa Timu ya Taifa ya vijana ya Rwanda chini ya miaka 23, Jimmy mulisa News Times

Timu ya Taifa ya Rwanda chini ya miaka 23 imeanza maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya DRC.

Matangazo ya kibiashara

Rwanda itachuana na DRC Novemba 14 kabla ya kurejeana Novemba 21 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo.

Mchezo baina ya Timu hizo utachezwa katika Uwanja wa Umuganda uliopo katika Wilaya ya Rubavu.

Kikosi cha Rwanda kitaongozwa na mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Rwanda na klabu ya APR Jimmy Mulisa.

Kikosi kamili cha Rwanda ni

Makipa : Gael Cyuzuzo, Fiacre Ntwali, Djihad Nzeyirwanda, and Adolphe Hakizimana.

Mabeki: Aime Placide Rwabuhihi, Prince Buregeya, Christian Ishimwe, Ange Mutsinzi, Claude Niyomugabo, Clement Niyigena, Marc Nkubana, Marc Nshimiyimana, Amza Runanira, Aimable Nsabimana and Derrick Ndahiro.

Viungo: Janvier Bonane, Valeur Nduwayo, Saleh Ishimwe, Djabel Manishimwe, Borde Cyitegetse, Sadjati Niyonkuru, Tresor Byunvuhore, Jean Baptiste Rugambwa, Savio Dominique Nshuti, Kevin Muhire, Patrick Mugisha and Freddy Muhoza.

Washambuliaji: Innocent Nshuti, Lague Byiringiro, Patrick Mugisha and Abeddy Biramahire.