GOR MAHIA-EVERTON-SOKA

Everton yaionyesha ubabe Gor Mahia

Klabu ya Kenya ya Gor Mahia.
Klabu ya Kenya ya Gor Mahia. Twitter. com/ Gor Mahia

Klabu ya Everton ilidhihirisha kuwa wamepiga hatua katika mchezo wa soka, baada ya kuishinda Gor Mahia ya Kenya mabao 4-0 katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki siku ya Jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo ilipigwa katika uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, katika mechi hiyo ya kihistoria kwa mabingwa wa soka nchini Kenya, ambao wameshinda ligi mara 17.

Everton ilipata bao la ufunguzi katika dakika ya 15 baada ya Ademola Lookman kumaliza pasi murua kutoka kwa Cenk Tosun, kabla ya Kieran Dowell kufunga bao la pili kupitia kichwa.

Mabao mengine yalifungwa na Nathan Broadhead na Oumar Niasse walipoingia katika kipindi cha pili.

Wachezaji wa Gor Mahia walionekana, walijitahidi mwanzoni mwa mechi hiyo lakini walielemewa kadiri mechi hiyo ilipokuwa inaendelea.

Mechi hiyo iliandaliwa na mfadhili wa klabu hizo kampuni ya Kenya SportPesa, inayohusika na ubashiri wa michezo.

Mwaka 2017, timu hizo mbili zilikutana jijini Dar es salaam na Everton kushinda kwa mabao 2-1.