KENYA-SOKA

Harambee Starlets yahitaji fedha kushiriki fainali za bara la Afrika

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets
Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets Harambee Starlets/Twitter.com

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, hueda ikalazimika kutoshiriki katika fainali za bara Afrika, zinazoanza wiki ijayo nchini Ghana, kwa sababu za kifedha.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Shirikisho la soka nchini humo FKF Nick Mwendwa, amesema timu inahitaji tiketi kufikia Jumanne wiki ijayo, ili kuwa na uhakika wa kusafiri.

Jumanne wiki ijayo, ndio makataa ya nchi hiyo kufahamu iwapo itashiki katika mashindano hayo au la.

“Timu yetu imekuwa ikifanya mazoezi kwa wiki mbili sasa lakini, hatujapata msaada wowote wa kifedha kutoka kwa serikali. Muda unakwenda sana na tuna hadi Jumanne, kuthibitisha iwapo tutasafiri,” amesema Mwendwa.

Iwapo Harambee Starlets, itashindwa kushirikishi katika mashindano hayo, ipo hatarini kuadhibiwa na Shirikisho la soka barani Afrika, CAF.