SOKJA-TANZANIA-AZAM FC
Azam yamsajili mchezaji Obrey Chirwa
Imechapishwa:
Klabu ya Azam FC imeanza kuimarisha kikosi chake baada ya kumsajili mchezji Obrey Chirwa kutoka nchini Zambia.
Matangazo ya kibiashara
Mchezjai huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na ameeleza matumaini yake ya kuisaidia klabu hiyo kutimiza lengo la kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.
Azam inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 30 baada ya kushuka uwanjani mara 11.
Dirisha dogo la usajili wa wachezaji katika Ligi ya Tanzania linatarajiwa kuanza hivi karibuni lakini Chirwa amesajili na Azam kwakuwa alikuw amchezaji huru.