RWANDA-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-AFCON

Kocha wa Amavubi atetea msimamo wa kuteua vijana katika mchezo wa Afcon

Kocha Mkuu wa Amavubi, Vincent Mashami
Kocha Mkuu wa Amavubi, Vincent Mashami Rwanda Times

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rwanda, Amavubi, Vincent Mashami ametetea msimamom wake wa kuteua wachezaji vijana wakati huu ikijiandaa kwa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Matangazo ya kibiashara

Mchezo baina ya Timu hizo utachezwa Novemba 18 Mjini Kigali huku Rwanda ikiwa haina matumaini yoyote ya kufuzu fainali baada ya kufanya vibaya katika mechi zake nne za kwanza katika Kundi H.

Mashami amesema uamuzi wake unalenga kutoa nafasi kwa wachezaji vijana kutoa mchango wao.

Baadhi ya wachezaji walioitwa kikosini kwa mara ya kwanza ni Rachid Kalisam Mohamed Mushimiyimana na Justin Mico.

Mchezo baina ya Rwanda na Afrika ya Kati utachezwa katika Uwanja wa Huye.

Mchezo wa mwisho kwa Rwanda utakuwa dhidi ya Ivory Coast ambao utachezwa Machi mwakani.