KLABU BINGWA AFRIKA-ESPERANCE-AL AHLY

Rekodi yaibeba Al Ahly, mechi ya marudiano klabu bingwa Afrika dhiai ya Esperance

Nyota wa Al Ahly Walid Azaro akichuana na mchezaji wa Espérance de Tunis, Chamseddine Dhaouadi katika mchezo wa kwanza wa fainali uliochezwa Novemba 2, 2018.
Nyota wa Al Ahly Walid Azaro akichuana na mchezaji wa Espérance de Tunis, Chamseddine Dhaouadi katika mchezo wa kwanza wa fainali uliochezwa Novemba 2, 2018. KHALED DESOUKI / AFP

Timu ya Esperance ya Tunisia leo usiku inaipokea Al Ahly ya Misri katika mechi ya marudiano ya Ligi ya mabingwa Afrika huku ikiwa nyuma kwa mabao 3-1. 

Matangazo ya kibiashara

Mchezo baina ya Timu hizo utachezwa katika Uwanja wa Olimpiki Rades uliopo katika Jiji la Rades nchini Tunisia.

Al Ahly iliwasili nchini Tunisia siku ya Ijumaa kwa ajili ya mchezo huo unaokutanisha miamba katika soka la Afrika.

Hata hivyo rekodi baina ya Timu hizo inaibeba Ahly ambao ni mabingwa mara nane wa michuano hiyo.

Timu hizo zimekutana mara 17 ambapo Esperance imeshinda mara tatu wakati wapinzani wao wameshinda michezo sita na kutoka sare mara nane.

 

Walid Azaro Chamssedine Dhuouad