Simba SC, Gor Mahia, Vipers na APR zafahamu wapinzani wao, michuano ya Klabu bingwa Afrika
Imechapishwa:
Ratiba ya Michuano ya klabu bingwa Afrika imetangazwa leo huku ikionyesha mabingwa wa soka Tanzania Simba SC kuwa watachuana na Mabingwa wa Eswatin, Mbabane Swallows.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mchezo wa kwanza baina ya Simba na Mbabane Swallows utachezwa ama tarehe 27 au 28 mwezi huu Jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki moja baadaye Mjini Mbabane.
Mshindi baina ya Simba na Mbababe atachuana nan mshindi baina ya Nkana ya Zambia na Uniao Desportiva Do Songo ya Msumbiji.
Mechi nyingine za awali ni kama ifuatavyo
Gor Mahia ya Kenya itachuana na Big Bullets ya Malawi
Asas Djibout Telecom ya Djibout itakumbana na Jima Abijafar ya Ethiopia
Orlando Piratees ya Afrika Kusini itakumbana na Light Star ya Ushelisheli
Le Messenger Ngozi ya Burundi itakuwa mwenyeji wa Ismailia ya Misri
AS Sonidep ya Niger itakuwa mwenyeji wa Zesco ya Zambia
ASFB ya Burkinafaso itakuwa mwenyeji wa Coton Sports ya Cameroon
APR ya Rwanda itakumbana na Club Africaine ya Tunisia
Al Hilal ya Sudan itacheza na JKU ya Zanzibar
Vipers ya Uganda itaanzia ugenini kwa kuchuana na El Merreikh ya Sudan
Katika Kombe la Shirikisho baadhi za awali zitakuwa kama ifuatavyo
Zimamoto ya Zanzibar itachuana na Kazier Chiefs ya Afrika Kusini
DC Motema Pembe itachuana na Les Anges De Fatima
AS Nyuki itaanzia ugenini dhidi ya Al Ahly Shandi ya Sudan
Mtibwa Sugar ya Tanzania itachuana na Nothern Dynamo ya Ushelisheli
Gambia Armed Forces itakumbana na San Pedro
Petro Atletico ya Angola itakuwa mwenyeji wa Orapa United ya Botswana