TAIFA STARS-LESOTHO-AFCON

Waamuzi wa burundi kuchezesha mechi ya Taifa Stars na Lesotho

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ni tegemeo la Tanzania katika harakati za kufuzu fainali za Afcon
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ni tegemeo la Tanzania katika harakati za kufuzu fainali za Afcon GOAL.COM

Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF limewataja waamuzi kutoka nchini Burundi kuchezesha mechi ya kuwania kufuzu fainali za Afrika baina ya Lesotho na Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo ya Kundi L itachezwa Oktoba 18, Mjini Maseru na itakuwa mechi muhimu kwa timu zote mbili.

Waamuzi walioteuliwa kuchezesha mchezo huo ni Mwamuzi wa kati, Thierry Nkurunziza ambaye atasaidiwa na waamuzi wasaidizi Jean Cloude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo.

Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi L ikiwa na alama 5 baada ya kucheza mechi nne, Uganda inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 10.

Kwa sasa Tanzania, imeweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo huo muhimu wa kufuzu fainali za Afrika.

Mchezo wa kwanza baina ya Timu hizo ulichezwa Juni mwaka 2017 katika Uwanja wa Azam Complex na kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.