KENYA-CECAFA-SOKA

CECAFA yaahirisha michuano kufuatia hatua ya chama cha soka Kenya

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Juni 28, 2018
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Juni 28, 2018 RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka

Baraza la Mchezo wa soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ,limeahirisha michuano ya mwaka huu kati ya timu za taifa. michuano hiyo itachezwa Julai mwakani, kwa mujibu wa CECAFA.

Matangazo ya kibiashara

Michuano hii ilikuwa imepangwa kufanyika nchini Kenya katika miji ya Machakos, Kisumu na Kakamega lakini chama cha soka nchini humo FKF, kimejiondoa kwa sababu za kifedha lakini pia ratiba ngumu ya michuano ya klabu bingwa na Shirikisho iliyotangazwa na CAF.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema baada ya Kenya kujiondoa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike mwisho wa mwezi huu, imekuwa ni vigumu kumpata mwenyeji mwingine haraka.

Michuano hiyo sasa itafanyika mwezi Julai mwakani, na itatunguliwa na ile ya klabu bingwa, maarufu kama Kagame Cup mwezi Juni.