Emerging Stars wajiweka kwenye nafasi nzuri
Imechapishwa:
Timu ya taifa ya soka ya Kenya, inayowajumuisha wachezaji wenye chini ya umri wa miaka 23, walianza vema kampeni ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika mwaka 2019 nchini Misri, baada ya kuifunga Mauritus mabao 5-0.
Emerging Stars, ilipata ushindi huo mkubwa katika mechi iliyochezwa siku ya Jumatano jioni latika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.
Mabao ya Johnston Omurwa, James Mazembe, Piston Mutamba, Sidney Lokale na Joseph Okumu yanaiweka Kenya katika nafais nzuri ya kufuzu katika hatua ya pili ya michuano hiyo, itakaporudiana na Mauritius tarehe 18 mwezi huu.
Matokeo zaidi:-
Burundi2-0 Tanzania
Ethiopia 4-0 Somalia
Rwanda 0-0 DRC
Uganda 1-0 Sudan Kusini
Ushelisheli 1-1 Sudan
Mataifa nane yatafuzu kushiriki katika fainali hiyo. Nigeria ndio mabingwa watetezi.