KENYA-SOKA

Harambee Stars waendelea kujinoa kuelekea fainali za barani Afrika mwaka 2019

Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA
Wachezaji wa Harambee Stars wakishangilia baada ya ushindi wa taji CECAFA Goal.com

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars, itakuwa na kambi ya wiki tatu barani Afrika, kuelekea fainali za barani Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Matumaini ya Kenya kufuzu katika fainali hiyo, yameongezeka, baada ya FIFA kuendelea kuifungia Sierra Leone na mchuano wake wa kufuzu uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumapili kuahirishwa.Kenya inatarajia kurejea katika mashindani hayo baada ya miaka 15. Waziri wa Michezo nchini humo Rashid Echesa amesema Kenya ina kikosi kizuri, hata iwapo kifungo cha Sierra Leone kitaondolewa, Harambee Stars itakuwa tayari kwa mchuano huo.

Mechi za mwishoni, mwa wiki hii zitaweka wazi timu zitakazofu katika fainali za AFCON:-

Comoros vs Malawi

Ushelisheli vs Libya

Afrika Kusini vs Nigeria

Uganda vs Cape Verde

Namibia vs Guinea-Bissau

Equitorial Guinea vs Senegal

Gabon vs Mali

Gambia vs Benin