UGANDA CRANES-AFCON2019-CAMEROON

Uganda Cranes ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kufuzu Afcon

Wachezaji wa Uganda cranes wakishangilia huku wakiwa wamembeba Kocha wao Sebastien Desabre baada ya kuishinda cape Verde bao 1-0, Novemba 17, 2018
Wachezaji wa Uganda cranes wakishangilia huku wakiwa wamembeba Kocha wao Sebastien Desabre baada ya kuishinda cape Verde bao 1-0, Novemba 17, 2018 Twitter/FUFA

Uganda imekuwa nchi ya kwanza kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kufuzu kushiriki fainali za Afrika, zitakazochezw amwkaani nchini Cameroon.

Matangazo ya kibiashara

Uganda imepata tiketi hiyo baada ya kuishinda Cape Verde kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Mandela Jijini Kampala.

Bao la Uganda lilifungwa na mchezaji Kaddu Patrick kunako kipindi cha pili cha mchezo huo ulioshuhudiwa na maelfu ya mashabiki.

Rais Yoweri Museveni ametumia ukurasa wake wa Twitter kuwamiminia salamu za pongezi Uganda Cranes na benchi la ufundi.

Hii ni mara ya saba kwa Uganda kufuzu kuchgeza fainali hizo, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 22017 zilipofanyika nchini Gabon.

Uganda inaongoza Kundi L ikiwa na alama 13, la leo Tanzania inaweza kuungana na Uganda ikiwa itaishinda lesotho katika mchezo utakaochezwa Mjini Maseru milango ya saa 11 kwa saa za Afrika Mashariki.