KENYA-GOR MAHIA-CAF-SOKA

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Gor Mahia aajiriwa na Black Leopards ya Afrika Kusini

Dylan Kerr, aliyekocho wa klabu ya Gor Mahia.
Dylan Kerr, aliyekocho wa klabu ya Gor Mahia. GOR MAHIA FC/twitter.com

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dylan Kerr ameajiriwa na klabu ya Afrika Kusini Black Leopards. Katika barua yake ya kujiuzulu ya tarehe 15 Novemba 2018, Kerr ameonyesha wazi kwamba atakuwa na nafasi nyingine ya kufundisha msimu mpya wa ligi na kuwashukuru viongozi wote wa klabu.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Uingereza, aliyejizulu kutoka Gor Mahia, anachukua nafasi ya Joel Masutha aliyeachia nafasi hiyo wiki iliyopita kwa sababu ya matokeo mabaya.

Mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia,Ambrose Rachier amethibitisha kupata barua ya kuacha kazi kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr.

Kocha huyo aliwashukuru pia wachezaji wa Gor Mahia kwa kumpatia ushirikiano na kuwataka waweke mawazo yao katika kazi yao ya soka.

Dylan Kerr anachukua uongozi wa klabu ambayo inashikilia nafasi ya 14 kati ya klabu 16 zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini, na kazi kubwa ni kuisaidia kupanda hadi katika nafasi za juu, katika msururu wa ligi kuu.