GHANA-CAMEROON-SOKA

Ghana kumenyana na Cameroon kuwania Kombe la bara Afrika

Mashabiki wa timu ya ya taifa ya soka ya Ghana Black Stars.
Mashabiki wa timu ya ya taifa ya soka ya Ghana Black Stars. REUTERS/Brian Snyder

Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Ghana, itacheza mechi yake ya pili dhidi ya Cameroon kutafuta ushindi wa pili, kuwania Kombe la bara Afrika, michuano inayoendelea jijini Accraa.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji walianza vema baada ya kuishinda Algeria bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Cameroon nao walianza kwa ushindi baada ya mechi yake ya kwanza, kuishinda Mali mabao 2-1.

Mechi nyingine hivi leo ni kati ya Mali na Algeria.

Kesho, Nigeria itamenyana na Zambia. Equitorial Guinea itachuana na Afrika Kusini.