UHISPANIA-MOROCCO-SOKA

Uhispania na Morocco wataka kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2030

Wachezaji wa soka wakati wa mechi katika uwanja wa Jose Rica Perez nchini Uhispania.
Wachezaji wa soka wakati wa mechi katika uwanja wa Jose Rica Perez nchini Uhispania. wikimedia.org

Nchi ya Uhispania imeandikia barua Morocco, kuomba ushirikiano pamoja na Ureno ili kuomba kwa pamoja kuwa wenyeji wa Kombe la dunia mnamo mwaka 2030.

Matangazo ya kibiashara

Ombi hili, limetolewa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wakati akiwa ziarani nchini Morocco siku ya Jumatatu.

Magazeti nchini Uhispania yanaripoti kuwa Morocco imekubali ombi hilo.

Uhispania imewahi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mara moja, mwaka 1982.

Morocco imejaribu kuomba kuwa mwenyeji wa Kombe la dunia la mwaka 1994, 1998, 2006, 2010 na 2026 bila mafanikio