MALI-GHANA-SOKA

Timu ya wanawake ya Mali yaiburuza Ghana kwa mabao 2-1

Mazoezi ya timu ya taifa ya soka ya wanawake "Les Elephants", Côte d’Ivoire.
Mazoezi ya timu ya taifa ya soka ya wanawake "Les Elephants", Côte d’Ivoire. Maureen Grisot/RFI

Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Mali, kwa upande wa wanawake, imefufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya mwondoano, kuwania taji la bara Afrika baada ya kuwafunga wenyeji Ghana mabao 2-1 katika mechi yake ya pili Jumanne wiki hii jijini Accra.

Matangazo ya kibiashara

Mechi ya kwanza, Mali ilianza vibaya baada ya kufungwa na Cameroon mabao 2-1.

Hata hivyo, Cameroon itandeleza ushindi katika mechi ya kundi A baada ya kushinda Algeria mabao 3-0.

Kwa matokeo haya, Cameroon wanaongoza kundi hilo kwa alama sita, Mali ni ya pili kwa alama tatu sawa na Ghana, huku Algeria ikiwa ya mwisho bila alama.

Mechi za kundi B, zinachezwa leo Jumatano, Nigeria inamenyana na Zambia, lakini Equitorial Guinea itajaribu kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Afrika Kusini.