BURUNDI-TANZANIA-CAF-SOKA

Timu zitakazoshiriki michuano ya mzunguko wa pili kwa vijana wasiozidi miaka 23 zajulikana

Timu ya taifa ya soka ya vijana wasiozidi miaka 23 ya Burundi Intamba mu Rugamba yafuzu katika duru ya pili baada ya kushinda Tanzania kwa bao la ugenini.
Timu ya taifa ya soka ya vijana wasiozidi miaka 23 ya Burundi Intamba mu Rugamba yafuzu katika duru ya pili baada ya kushinda Tanzania kwa bao la ugenini. F.F.B ‏ @BurundiFF/twitter

Michuano ya mzunguko wa kwanza, kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika katika mchezo wa soka kwa vijana wasiozidi miaka 23 nchini Cairo mwaka ujao, ilimalizika Jumanne wiki hii na sasa tayari ratiba imeshapangwa kwa michuano ya mzunguko wa pili.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kushinda Tanzania kwa bao la ugenini, Burundi itamenyana na Congo Brazaville, licha ya kushinda mabao 3-1, vijana wa Tanzania waliondolewa kwa sababu Burundi walikuwa wamepata ushindi nyumbani wa mabao 2-0 na kuruhusu bao katika mechi ya Jumanne kuliwaharubia mambo.

Kenya itacheza na Sudan, baada ya kufanikiwa kuishinda Mauritius kwa jumla ya mabao 8-1, huku Sudan ikiilemea Ushelisheli kwa jumla ya mabao 2-1.

DRC nayo itamenyana na Morocco, baada ya kuilemea Rwanda kwa jumla ya mabao 5-0.

Ethiopia nayo itamenyana na Mali. Mechi hizi, zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu latika mzunguko wa tatu na wa mwisho, ili kutafuta timu nane bora kutafuta ubingwa wa Afrika.