COTE D'IVOIRE-SOKA

Didier Drogba astaafu kucheza soka

Didier Drogba.
Didier Drogba. Christian Petersen / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa timu ya taifa ya soka ya Cote d'Ivoire Didier Drogba, amesema anastaafu kucheza soka, baada ya zaidi ya miaka 20 katika viwanja vya mchezo wa soka.

Matangazo ya kibiashara

Drogba mwenye umri wa miaka 40, anastaafia katika klabu ya Phoenix Rising nchini Marekani.

Alianza kucheza ya kulipwa mwaka 1998 katika klabu ya Le Mans nchini Ufaransa, kabla ya kwenda katika klabu ya Guingamp na baadaye kwenda Marseille.

Didier Drogba, wakati wa ushindi wa Chelsea, katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2012.
Didier Drogba, wakati wa ushindi wa Chelsea, katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2012. ADRIAN DENNIS / AFP

Hata hivyo, umaarufu wake ulifahamika sana katika klabu ya Chelsea nchini Uingereza, alikofunga mabao 164 katika mechi 341.

Aliichezea timu yake ya taifa kati ya mwaka 2002-2014 na kuichezea mechi 104 na kufunga magoli 65, rekodi ambayo bado anaishikilia.

Didier Drogba wakati akiichezea klabu ya Montreal.
Didier Drogba wakati akiichezea klabu ya Montreal. Trevor Ruszkowski-USA TODAY Sports