NIGERIA-ZIMBIA-SOKA

Nigeria wawaadhibu Zambia kwa mabao 4-0

Timu ya Soka ya Wanawake ya Nigeria
Timu ya Soka ya Wanawake ya Nigeria NGSuper_Falcons/Twitter

Mabingwa watetezi wa taji la bara Afrika katika mchezo wa soka kwa upande wa wanawake, Super Falcons ya Nigeria, hatimaye wamefufua matumaini ya kusonga mbele katika fainali za mwaka huu zinazoendelea jijini Accra nchini Ghana, baada ya kuifunga Zambia mabao 4-0 katika mechi yake ya pili siku ya Jumatano usiku.

Matangazo ya kibiashara

Huu ni ushindi muhimu kwa Nigeria, ambao walianza vibaya michuano hii baada ya kufungwa na Afrika Kusini bao 1-0.

Hata hivyo, mambo yanaendelea kuwa mabaya kwa Equitorial Guinea ambao walipoteza mechi yake ya pili baada ya Afrika Kusini kupata karamu ya mabao 7-1.

Baada ya matokeo hayo, Afrika Kusini inaongoza kundi la B, kwa alama 6, huku Nigeria na Zambia zikiwa na alama tatu.

siku ya Ijumaa kutakuwa na michuano ya kumaliza kundi A, Cameroon watachuana na Ghana, huku Algeria wakicheza na Mali.