LIBERIA-SOKA

Wachezaji wa timu ya taifa ya Liberia kulipwa mshahara kila mwezi

Rais wa Liberia George Weah.
Rais wa Liberia George Weah. REUTERS/Thierry Gouegnon

Rais wa Liberia George Weah, amesema anafikiri kuwajumuisha wachezaji wa timu ya taifa ya soka katika orodha ya wafanyakazi wa serikali wanaostahili kulipwa mshahara kila mwezi.

Matangazo ya kibiashara

Iwapo atatekeleza hilo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa taifa la kwanza duniani kuwalipa mshara wachezaji mshahara kila mwezi.

Weah ambaye ni mchezaji wa zamani wa soka wa nchi yake, amekuwa akisema wachezaji wanajitoa na kufanya bidhaa kwa ajili ya taifa lao bila kupata chochote na mfumo huu, utawatia moyo.

Hivi karibuni, timu taifa ya Liberia iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu fainali ya bara Afrika mwaka 2019 nchini Camerooon.