MISRI-SOKA-CAF

Issa Hayatou na Hicham El Amrani wajibu baada ya kuhukumiwa

Issa Hayatou (Cameroon) na Hicham El Amrani (Morocco).
Issa Hayatou (Cameroon) na Hicham El Amrani (Morocco). ISSOUF SANOGO / AFP

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou na aliyekuwa Katibu Mkuu Hicham El Amrani wametozwa faiani ya Dola Milioni 27.9 kila mmoja na Mahakama ya Uchumi nchini humo Misri (EEC).

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo imesema kuwa wawili hao walivunja sheria ya nchi hiyo kwa kutia saini mkataba wa Dola Bilioni Moja kati ya CAF na kampuni ya Ufaransa ya Lagardere mwak 2015.

Sheria ya Misri, inasema kuwa, kupata mkataba huo, lazima uwe wazi kwa kila mmoja lakini haikuwa hivyo.

Hata hivyo, El Amrani na Hayatou wamesema kuwa, watakata rufaa kuhusu faini hiyo.

Aidha, wanasema kuwa kesi hiyo imechochewa kisiasa.